Wanafunzi wakwaruzana vikali na polisi Chile

Maandamano kama hayo yamefanyika katika miji mingine tofauti Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Maandamano kama hayo yamefanyika katika miji mingine tofauti

Wanafunzi waliokuwa wakiandamana nchini Chile kupinga mabadiliko ya elimu wamekwaruzana vikali na vikosi vya usalama.

Mwezi machi katika mji mkuu Santiago, wanafunzi walirusha mawe kwa vikosi vya polisi ambavyo vilikuwa vikitumia gesi ya machozi na maji ya kuwasha kuwatawanya.

Maandamano kama hayo pia yamefanyika katika miji mingine miwili.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Maandamano hayo hayana dalili za kumalizika

Rais wa Chile Michelle Bachelet ameamuru kuongeza idadi ya wanafunzi watakaopokea mkopo kwa elimu ya juu hii ikiendana na ukuaji wa uchumi.

Lakini wanafunzi wanataka kupata mkopo wa kusoma masomo ya ziada.