UN yaonya watoto kutumiwa na Boko Haram, kushambulia

Shambulio la Bomu lililofanywa na Boko Haram

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Shambulio la Bomu lililofanywa na Boko Haram

Ripoti ya Umoja wa Mataifa imesema katika kipindi cha miezi mitatu mwaka huu, watoto walitumiwa kufanya mashambulizi 27 ya kujitoa mhanga katika nchi za Nigeria, Niger, Chad na Cameroon.

Idadi hiyo ni karibu na yale yaliyofanywa katika mwaka mzima wa 2016.

Watoto wengi wanaotumiwa kufanya mashambulizi hayo ni wasichana, wakilenga maeneo ya umma na vizuizzi vya kijeshi.

Umoja wa Mataifa umelaani hila na ulazimishaji unaofanya na kundi hilo la Boko Haram kuwatumia wanawake na watoto kufanya mashambulizi hayo ya mabomu.

Ripoti zinasema watoto wanapaswa kutazamwa kama waathirika wa matukio hayo na sio watenda kosa.