Wapenzi wa jinsi moja kuhamishwa Chechnya

Chechnya yapinga wanaofanya mapenzi ya jinsi moja

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Chechnya yapinga wanaofanya mapenzi ya jinsi moja

Wanaharakati wa kutetea haki za watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja nchini Urusi wanapanga kuwahamisha wanaume wanaojihusisha na mapenzi hayo ambao wanakabiliwa na mateso adhabu na hata vifo katika Jamhuri ya Chechnya iliyoko kusini mwa Urusi.

Natalia Poplevskaya kutoka katika mtandao wa LGBT mjini Saint Petersburg ameiambia BBC kwamba tangu wimbi la kukamatwa kwa watu hao kuanza Februari mwaka huu takriban watu 100 wamewekwa vizuizini, huku wengine wamekamatwa kwa kuwa tu, majina yao yako kwenye simu za marafiki zao ambao wanajihusisha na mapenzi hayo.

Amesema baadhi yao wameteswa. Huku wengine wakikabidhiwa kwa familia zao kwa ajili ya kuwaua ili wasitambulike na kupatwa na aibu.

Kiongozi wa Chechnya Ramzan Kadyrov amekana madai hayo, akisema kwamba hakuna watu wenye mapenzi ya jinsia moja Chechnya.