Aliyesema Hitler hakutumia sumu aomba radhi Marekani

Katibu wa maswala ya habari nchini Marekani Sean Spicer
Maelezo ya picha,

Katibu wa maswala ya habari nchini Marekani Sean Spicer

Katibu wa maswala ya habari nchini Marekani Sean Spicer ameaomba radhi baada ya kusema kuwa Adolf Hitler hakutumia kemikali za sumu wakati wa vita vya pili vya dunia.

Nilifananisha vibaya mauaji ya halaiki ya wayahudi ,kwa hivyo naomba msamaha.

Ilikuwa makosa makubwa kufanya hivyo.Wakosoaji wanasema kuwa gesi ilitumika katika kuwaua Wayahudi na wengine katika mauaji hayo ya halaiki.

Bwana Spicer amekuwa akikosoa hatua ya Urusi kuunga mkono serikali ya Syria.

Ikulu ya Whitehouse inasema kuwa Urusi imekuwa ikijaribu kujiondolea lawama kuhusu shambulio la kemikali ya sumu lililowaua watu 89.

Vitengo vya kijasusi nchini Marekani vinasema kuwa Serikali ya Syria ilitumi silaha za kemikali wakati wa mashambulio ya angani.

Syria imekana hilo na badala yake kuwalaumu waasi ambao inasema wamekuwa wakihifadhi slihaha za sumu ambazo zilishambuliwa wakati wa uvamizi huo.