Malalamishi yatolewa kuhusu tangazo la mwanamitindo mwembamba

Mamlaka kuu ya kudhibiti viwango vya matangazo (ASA) ilikamilisha kuwa mwanadada huyo haonekani kuwa "ana uwembamba kupita kiasi"

Chanzo cha picha, PA

Maelezo ya picha,

Mamlaka kuu ya kudhibiti viwango vya matangazo (ASA) ilikamilisha kuwa mwanadada huyo haonekani kuwa "ana uwembamba kupita kiasi"

Tangazo la kibiashara la mtindo wa nguo katika kampuni ya Selfridges, imeingiliwa kati na kampuni kuu linalodhibiti maswala ya matangazo, baada ya malalamiko kutokea kuwa mwanamitindo aliyetumika katika tangazo hilo ni mwembamba na anaonekana kama "asiye na afya".

Barua pepe ya tangazo hilo kutoka kwa idara ya maduka hayo mwezi Januari mwaka huu, linamuonyesha mrembo akisimama kidete akivalia vazi la rangi ya samawati. Lilimfanya msomaji mmoja kulalamika kuwa mwanamitindo huyo ni mwembamba zaidi na kuuliza iwapo tangazo hilo lilifaa kutumika

Lakini mamlaka kuu ya kudhibiti viwango vya matangazo (ASA) ilikamilisha kuwa mwanadada huyo haonekani kuwa "ana uwembamba kupita kiasi".

Chanzo cha picha, PA

Maelezo ya picha,

Maduka ya Selfridges, yanasema kuwa hakusimama ipasavyo ili kuficha uwembamba alio nao.

Maduka ya Selfridges, yanasema kuwa hakusimama ipasavyo ili kuficha uwembamba alio nao.

Kampuni hiyo aidha, inasema kuwa licha ya kukuri kuwa mwana mitindo huyo ni mwembamba, mtazamo wa jumla wa ummaof kuhusiana na uzani wake, na ikiwa mwanadada huyo anaonekana hana afya au mwembamba, uwembamba ndilo swala linaloangaziwa.