MCA Tricky anatumia umaarufu wake kusaidia vijana wa mitaani

Leo ulimwengu unaadhimisha siku ya kimataifa ya watoto wanaoishi mitaani. Kuangazia siku hii, mwandishi wa BBC Anthony Irungu amezungumza na mchekeshaji maarufu kutoka Kenya anayejulikana kwa jina la usanii 'MCA Tricky' kuhusu maisha yake mitaaani na jinsi anavyotumia umaarufu wake kuwasaidia vijana wengine mitaani.