Kiongozi wa upinzani Zambia afunguliwa mashtaka ya uhaini

Hakainde Hichilema alikamatwa siku ya Jumatatu usiku baada ya polisi kuvamia nyumba yake mjini Lusaka.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Hakainde Hichilema alikamatwa siku ya Jumatatu usiku baada ya polisi kuvamia nyumba yake mjini Lusaka.

Kiongozi wa upinzani nchini Zambia Hakainde Hichilema, amefunguliwa mashtaka ya uhaini, kwa mujibu wa mkuu wa polisi nchini humo.

Alikamatwa kufuatia madai kuwa msafara wake ulikataa kuupisha ule wa rais Edgar Lungu.

"Imebainika kuwa kiongozi huyo wa upinzani alipuuza maagizo ya polisi ya kuondokea msafara wa raisip, na hivyo kuyaweka maisha ya rais hatarini, mkuu wa polisi Kakoma Kanganja, aliliambia shirika la Reuters.

Alikamatwa siku ya Jumatatu usiku baada ya polisi kuvamia nyumba yake mjini Lusaka.

Mkewe amekiambia kituo cha runinga cha nchi hiyo Muvi TV kuwa polisi walitaka kumuua mumewe.