Panda wawili wawasili Uholanzi tokea China

Wamepokelewa kwa heshima nchini Uholanzi
Maelezo ya picha,

Wamepokelewa kwa heshima nchini Uholanzi

Panda wawili wakubwa wamewasili nchini Uholanzi baada ya safari ya saa 10 kutoka mji wa Chengdu China.

Xing Ya na mwenzake, Wu Wen, waliwasili uwanja wa ndege wa Schiphol na kisha kupelekwa katika hifadhi ya makumbusho ya Ouwehands.

Panda hao walikuwa zawadi kwa familia ya kifalme ya Uholanzi wakati walipotembelea nchi ya China mwaka 2015.

Wamepewa visa za nchi za Schengen ambazo wanaweza kuzungushwa nchi mbalimbali za Ulaya.