Msafara wa Wafungwa washambuliwa Chad, 10 wauawa

Ramani ya Chad
Watu 10 wameuawa nchini Chad katika shambulio lililofanywa kwenye msafara uliokuwa ukisafirisha wafungwa.
Mauaji hayo yametokea wakati walinzi walipokuwa wakiwa hamisha watu wanaoshikiliwa kutoka mji mkuu wa nchi hiyo Ndjamena kwenda kwenye gereza lenye ulinzi mkali kaskazini mwa nchi.
Walinzi wawili ni miongoni mwa waliouawa.
Mwandishi wa BBC nchini humo amesema shambulio hilo ni matokeo ya uhasama baina ya koo mbili.
Ulinzi umeimarishwa katika eneo la chumba cha kuhifadhia maiti mjini Ndjamena ambako miili hiyo imehifadhiwa.