Wakaazi wa India waghadhabishwa na malipo ya rupia milioni moja kwa kichwa cha waziri mkuu Mamata Banerjee

Bwana Varshney aliwalaumu polisi kwa kuwashambulia waja kikatili na kusema kuwa hatua hiyo ilitolewa na Bi Banerjee ambaye alitajwa kuwa "shetani"

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Bwana Varshney aliwalaumu polisi kwa kuwashambulia waja kikatili na kusema kuwa hatua hiyo ilitolewa na Bi Banerjee ambaye alitajwa kuwa "shetani"

Wakaazi wa India wamejawa na ghadhabu baada ya mshiriki wa chama tawala nchini BJP kutoa rupia milioni 1.1 ($17,018; £13,622) kwa yule atakayemletea kichwa cha waziri mkuu wa jimbo la magharibi mwa Bengal Mamata Banerjee.

Yogesh Varshney alitoa tishio hilo baada ya polisi kuvunja mkutano hivi karibuni wa kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa mungu wa kihindi Hanuman.

Bwana Varshney aliwalaumu polisi kwa kuwashambulia waja kikatili na kusema kuwa hatua hiyo ilitolewa na Bi Banerjee ambaye alitajwa kuwa "shetani"

Chanzo cha picha, Voice Of Ram

Maelezo ya picha,

Mwanasiasa Yogesh Varshney aliyetaka kuuawa kwa waziri mkuu huyo wa Bengal

Hata hivyo chama cha BJP kilikana tangazo hilo.

"Nimekashifu tangazo hilo. Serikali yaweza kuchukua hatua inayofaa dhidi yake". Mukhtar Abbas Naqvi, waziri wa shirika na pia naibu wa rais katika chama cha Bharatiya Janata alisema bungeni siku ya Jumatano.

Bi Banerjee ni mwanasiasa maarufu aliyetajwa kati ya watu 100 wenye ushawishi mkubwa duniani katika nakala ya Times mwaka wa 2012.

Bwana Varshney ni mshiriki wa mrengo wa vijana katika chama tawala cha Bharatiya Janata

Ripoti zilisema kuwa polisi walikataa kuwapa ruhusa ya mkutano huo kufanyika siku ya Jumapili katika jiji la Birbhum, kilomita 180 kutoka kwa mji mkuu Kolkata ( iliyokuwa Calcutta) na kuivunja mkutano huo kwa kutumia nguvu ilipojaribu kuingia eneo hilo linaloongozwa na waislamu.

Bwana Varshney alisema kuwa serikali ya Bi Banerjee's inawalenga waja wa kihindi.

"Atakayeniletea Kichwa cha Mamata Banerjee... Nitamlipa rupia milioni 1.1," alisema siku ya Jumanne, akimtaja waziri mkuu kama "shetani"

Chama cha Bi Banerjee cha All India Trinamool Congress limeikashifu vikali tangazo hilo na kudai kushikwa kwa bwana Varshney.

Wahindi wengi pia walienda kwa mitandao ya kijamii kukashifu vitisho hivyo.

Chanzo cha picha, @SHREYATERESITA

Maelezo ya picha,

Wahindi wengi katika mitandao ya kijamii wamekukashifu vitisho hivyo.