Mkenya ashinda kiti cha Seneta Australia

Bi Lucy Gachui

Chanzo cha picha, ABC

Maelezo ya picha,

Bi Lucy Gachui

Mwanamke mmoja mzaliwa wa Kenya Lucy Gichuhi, anatazamiwa kuwa mtu wa kwanza mwenye asili ya kiafrika kuketi kwenye baraza la bunge la seneti lenye waakilishi 76, ikiwa uteuzi wake utathibitishwa na mahakama kuu, gazeti la The Guardian limeripoti.

Bunge la Seneti la Australia, lina nguvu ya kurekebisha au kumtimua mbunge.

Alipata kiti hicho baada ya mwenzake kutoka chama cha Family First -FF, Bw Bob Day, ambaye awali alishinda kwenye uchaguzi, kulazimishwa kuachia kiti hicho.

Bi Gichuhi, ambaye ni mhasibu na wakili, alihamia Australia mnamo mwaka 1999 na akapata uraia wa nchi hiyo miaka miwili baadaye, hii ni kwa mjibu wa taarifa kutoka kwa runinga ya ABC.

ABC imemnukuu akisema:

"Ninashukuru kwa heshima kubwa kwa kupewa nafasi hii ya kuwatumikia wa-Australia....ninalichukulia kama fursa kubwa ya kulitumikia taifa hili kubwa."

Tangazo la mtandaoni, kwamba angekabiliwa na upinzani ikiwa ingebainika wakati fulani kuwa ana uraia wa mataifa mawili, lakini alisema kuwa "ana haki ya kutumikia".