Drogba kumiliki klabu ya Phoenix Rising Marekani

Drogba akishangiliwa na umati wa watu huko Toronto alipoingia uwanjani katika michuano ya mkondo wa kwanza

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Drogba akishangiliwa na umati wa watu huko Toronto alipoingia uwanjani katika michuano ya mkondo wa kwanza

Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea na Ivory Coast Didier Drogba amejiunga na timu ya soka inayocheza katika ligi kuu ya kandanda nchini Marekani- Phoenix Rising kama mchezaji na pia mmiliki mwenza.

Drogba mwenye umri wa miaka 39, hajasakata kabumbu tangu alipoondoka katika klabu ya Montreal Impact mwezi Novemba mwaka jana.

Ataanza kama mchezaji, lakini pia amejiunga na kampuni tanzu ya Phoenix- "MLS kama mmiliki wake".

"ili kumiliki timu ya soka na pia kuwa mchezaji wake, ni jambo lisilo la kawaida, lakini itakuwa jambo la kupendeza sana," Drogba amesema.

"Ni mabadiliko mazuri kwa sababu nataka kuendelea kusakata kabumbu, lakini nakaribia miaka 40, na ni jambo bora kwangu kujiandaa kwa taaluma yangu ya baadaye.."

Timu ya Phoenix ndio mwanzo inaanza msimu wao wa nne katika kanda ya magharibiwa USL, mbayo inajumuisha mechi ya pili ya mfumo wa ligi kuu nchini Marekani.

Chanzo cha picha, Rex Features

Maelezo ya picha,

Mara ya mwisho Drogba akiichezea timu ya Montreal Impact

Timu ya Arizona, inatarajia kuwa katika mojawepo ya mipango ya upanuzi wa timu za MLS katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.

"Nimepata maombi kadhaa kutoka China na Uingereza- katika ligi zote kuu na vilevile mchuano wa vilabu bingwa barani Ulaya- lakini maombi hayo yote yananitaka tu kama mchezaji," Drogba ameiambia kipindi cha runinga na ligi kuu.

"Hii imekuwa maombi bora kwa sababu ilikuwa bora kwangu mimi, kufikiria namna ya kucheza, kwa sababu naipenda, lakini pia kuvuka hadi kiwango kingine cha taaluma yangu mpya."