Gazeti latumika katika taarifa bandia Kenya

Mgombea kiti cha Ugava, kaunti ya Busia, Paul Otuoma

Chanzo cha picha, Twiter

Maelezo ya picha,

Mgombea kiti cha Ugava, kaunti ya Busia, Paul Otuoma

Huku vyama vikuu vya kisiasa nchini Kenya, vikianza rasmi shughuli za uteuzi wa wagombea wake wa viti vya udiwani, ubunge, wawakilishi wa kina mama, useneta na ugavana, mara nyingi zoezi hilo huwa lenye ushindani mkubwa, kabla ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu.

Kenya inajiandaa kwa uchaguzi mkuu utakaofanyika mwezi Agosti mwaka huu.

Mgombea mmoja wa upinzani anayewania kiti cha ugavana katika kaunti ya Busia, magharibi mwa nchi hiyo, ameshtushwa kupata magazeti ya Daily Nation; mojawepo ya kampuni kubwa ya habari Afrika mashariki na kati, iliyochapisha na kusambaza taarifa feki, katika eneo hilo - inayodai kuwa amekihamia chama tawala cha muungano wa Jubilee, chama ambacho hakina uungwaji mkono katika kaunti hiyo.

Paul Otuoma, anaonekana akishikilia bango yenye picha yake ya kuomba kura kwa tiketi ya chama cha Jubilee, na pia nakala ya gazeti la zamani la Daily Nation yenye taarifa kuu kwenye ukurasa wa mbele wa inayosema kuwa amekihamia chama cha Jubilee.

Kichwa cha gazeti hilo sio la sasa, bali gazeti la zamani la Daily Nation, iliyoandika kwamba Bw Otuoma alikuwa amekihamia chama cha Jubilee, lakini alirejea tena ndani ya chama cha ODM cha muungano wa NASA, huku akipania kumuondoa gavana wa sasa wa eneo hilo Bw Sospeter Ojaamong.

Ripoti hiyo ya Daily Nation kwamba, mpinzani wa Otuona ambaye ni gavana wa sasa wa kaunti ya Busia, Sospeter Ojaamong, anaonekana kutilia mkazo taarifa hizo bandia, kwa kusema kuwa "Dkt Otuoma amekihama chama cha ODM na kuingia Jubilee".

Kampuni ya Nation Media Group, inayomiliki gazeti la Daily Nation, imetoa taarifa inayoeleza kutumika vibaya kwa gazeti lake kwa maslahi ya kisiasa, huku ikisema kuwa imefahamisha vyombo vya usalama kuchunguza taarifa hizo.

Chanzo cha picha, Twiter

Maelezo ya picha,

Taarifa ya Nation Media Group kwa vyombo vya Habari