Mtoto wa miaka 8 aendesha gari kununua chakula duka la McDonald's

Mtoto wa miaka 8 aendesha gari kununua chakula

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mtoto wa miaka 8 aendesha gari kununua chakula

Mtoto mmoja mvulana mwenye umri wa miaka minane katika jimbo la Ohio, aliendesha gari akiwa na dadake mdogo hadi duka la McDolad's baada ya kujifunza kuendesha gari kupitia mtandao wa YouTube.

Jarida na Morning Journal la Ohio lilisema kuwa polisi walipigiwa simu kutoka kwa wenyeji kuhusu mtoto ambaye alikuwa akindesha gari mjini.

Wafanyakazi katika mkahawa wa McDolad's walidhani kuwa ulikuwa ni mchezo wa kuigiza wakati mtoto huyo alisimamisha gari kwenye dirisha kununua chakula.

Mtoto huyo alifuata shera zote za barabara, mtu mmoja aliyeshuhudia alisema.

"Hakugonga chochote njiani, polisi Jacob Koeher kutoka kijiji cha East Palestine alisema.

Mtoto huyo aliwaambia polisi kuwa alijifuza kuendesha gari kwa kutazama video kwenye mtandao wa YouTube.

Inaripotiwa kuwa wazazi wa watoto walikuwa nyumbani wamelala wakati watoto hao waliamua kuchukua funguo za gari.

Baadaye wazazi wao waliitwa kuwachukua na hakuna mashtaka yaliyofunguliwa.