Assad: Shambulizi la kemikali lilikuwa ni uwongo asilimia 100

Assad anasema shambulizi la kemikali lilikuwa uwongo asilimia 100

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Assad anasema shambulizi la kemikali lilikuwa uwongo asilimia 100

Rais wa Syria Bashar-al Assad, anasema kuwa ripoti za shambulizi la silaha za kemikali lililofanywa na jeshi lake lilikuwa ni uwongo kwa asilimia mia moja.

Katika mahojiano ya kipekeke na kituo cha Agence France-Presse, Assad alisema kuwa hakukuwa na amri ya kufanywa shambulizi lolote.

Zaidi ya watu 80 waliuawa katika mji unaoshikiliwa na waasi wa Khan Sheikhoun tarehe 4 mwezi Aprili, na mamia kupata matatizo yaliyosababishwa na kile kinachotajwa kuwa shambulizi la kemikali.

Walioshuhudia walisema kuwa waliona ndege zikishambuaia mji huo lakini Urusi inasema kuwa ghala la silaha la waasi ndilo lilishambuliwa.

Picha za kushagaza zilionyesha waathiriwa wengi wao wakiwa ni watoto wakitokwa na pofu mdomoni.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Assad anasema shambulizi la kemikali lilikuwa uwongo asilimia 100

Walioathirika walipelekwa hospitalini nchini Uturuki inayompinga rais Assad

Tangu wakati huo Uturuki ilisema ina ushahidi kuwa silaha za kemikali zilitumiwa,.

Bwana Assad anasema kuwa nchi za magharibi zilibuni taarifa hiyo kama kisingizio cha kufanya shambulizi la ndege katika kituo cha wanahewa wa Syria, shambulizi hilo lilifanyika siku chache baadaye.

Urusi, mshirika mkubwa wa Syria iliwagadhabisha Marekani, Uingereza na Ufaransa siku ya Jumatano, kwa kupinga msuada ambao ungeruhusu serikali ya Assad kutoa ushirikiano kwa uchunguzi kuhusu kile kilichotokea.