Ashtakiwa kwa tuhuma za Ukeketaji Marekani

Yusra Warsama akiigiza kama mwanamke aliyekeketwa
Maelezo ya picha,

Yusra Warsama akiigiza kama mwanamke aliyekeketwa

Daktari nchini Marekani ameshtakiwa kwa tuhuma za kuendesha zoezi la kuwakeketa wasichana wadogo.

Inaaminika kuwa mashtaka hayo ni ya kwanza ya aina yake nchini humo.

Waendesha mashtaka katika jimbo la Michigan wamesema Dokta Jumana Nagarwala kwa miaka 12 amekuwa akiendesha zoezi la kuwakeketa watoto wa kike wenye umri ya kati ya miaka sita mpaka nane.

Amekuwa akichunguzwa baada ya mamlaka nchini humo kupewa taarifa na wasamaria wema.

Iwapo atakutwa na hatia Dokta Nagarwala atakabiliwa na kifungo cha juu gerezani.

Ukeketaji wanawake ni jambo ambalo limekuwa ni kinyume cha sheria nchini Marekani tangu mwaka 1996.