'Dandora Hip Hop City': Mwanamuziki Juliani anatumia Hiphop kusaidia vijana

'Dandora Hip Hop City': Mwanamuziki Juliani anatumia Hiphop kusaidia vijana

Mtaa wa Dandora mashariki mwa Nairobi unasemekana kuwa miongoni mwa mitaa hatari Zaidi nchini Kenya kwa sababu ya magenge ya wahalifu yanayojumuisha vijana wadogo.

Lakini pia Mtaa huo unajulikana kama chimbuko la muziki wa Hip Hop nchini humo, kupitia kwa makundi ya muziki kama vile 'Ukoo Flani Mau Mau' .

Anthony Irungu amezungumza na mwanamuziki maarufu Afrika mashariki, Juliani - mwenyeji wa Dandora, kuhusu anavyotumia muziki huo wa hip hop kubadilisha maisha ya vijana kupitia mradi wake 'Dandora Hip Hop City'.