Wanajeshi wa Marekani kuwafunza wanajeshi wa Somalia

Wanajeshi wa Kenya watumwa nchini Somalia kuwafunza wanajeshi wa taifa hilo
Maelezo ya picha,

Wanajeshi wa Kenya watumwa nchini Somalia kuwafunza wanajeshi wa taifa hilo

Marekani imewatuma wanajeshi wake nchini Somalia kusaidia kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa serikali wanaokabiliana na wapiganaji wa Al Shabaab.

Hii ndio mara ya kwanza Marekani inatuma wanajeshi wake tangu mwaka wa 1994.

Kumekua na kundi dogo la wanajeshi wa Marekani wanaotoa ushauri katika vita dhidi ya ugaidi nchini Somalia.

Marekani iliwapoteza wanajeshi 18 katika makabiliano na makundi ya wapiganaji baada ya helikopta yao kudunguliwa mwaka wa 1993.

Afisa wa serikali ya Marekani amesema hatua ya sasa imefuatia ombi la serikali ya Somalia.