Mchekeshaji Ayeiya poa poa nchini Kenya afariki

Mchekechaji Ayeiya poa poa nchini Kenya afariki Haki miliki ya picha Makori Nyambane
Image caption Mchekechaji Ayeiya poa poa nchini Kenya afariki

Jamii ya wachekeshaji nchini Kenya inaomboleza kifo cha ghafla cha mmoja wao.

Habari zimesema kuwa mchekeshaji maarufu wa kipindi cha Churchil Emmanuel Makori Nyambane aka Ayeiya Poa Poa amefariki.

Ayeiya Poa Poa kama anavyojulikana na mashabiki wake alihusika katika ajali mbaya ya barabarani karibu na chuo kikuu cha Catholic University CUEA.

Alifariki papo hapo.

Huwezi kusikiliza tena
MCA Tricky anatumia umaarufu wake kusaidia vijana wa mitaani

Mchekeshaji huyo alikuwa na mkewe, msanii Maina Olwenya na mchekeshaji mwengine Paul Wakimani Ogutu.

Ayeiya alikuwa akijulikana kwa ubunifu wake na mzaha ambao uliwawacha mashabiki wengi wakicheka hadi kuumwa na mbavu.