Urusi yaandaa mazungumzo ya amani Afghanistan huku Marekani ikisusia

Marekani imesusia mazungomzo hayo baada ya Urusi kulialika kundi la wapiganaji wa Taleban
Maelezo ya picha,

Marekani imesusia mazungomzo hayo baada ya Urusi kulialika kundi la wapiganaji wa Taleban

Urusi inaandaa mazungumzo ya amani kuhusu Afghanistan siku ya Ijumaa.

Marekani imesusia mazungumzo hayo kwa sababu Urusi imealika kundi la Taliban.

Mamlaka za Washington zinasema kualika Taliban ni kulipa kundi hilo hadhi ambayo haistahili.

Wadadisi wanasema Marekani inachukulia uhusiano kati ya Taliban na Urusi kama hatua za kuhujumu shughuli za shirika la NATO nchini Afghanistan.

Mataifa ya India, Iran , India na nchi nyingine za bara Asia zinahudhuria mazungumzo ya Moscow.

Mwandishi wa BBC amesema Urusi imeanza kuwa na ushawishi nchini Afghanistan tangu kundi la Islamic State kuanza operesheni zake nchini humo.