Wapiganaji 90 wa IS wadaiwa kuuawa na bomu kubwa la US

Bomu kubwa la Marekani lililoangishwa katika maficho ya IS
Maelezo ya picha,

Bomu kubwa la Marekani lililoangishwa katika maficho ya IS

Maafisa wa usalama nchini Afghanistan wanasema kuwa zaidi ya wapiganaji 90 wa kundi la kigaidi la Islamic State waliuawa na bomu kubwa lililodondoshwa na Marekani mnamo Alhamisi.

Kiasi hicho ni mara mbili ya kiasi kilichokuwa kimekisiwa awali.

Islamic State wamekanusha kuwa walimpoteza mtu ye yote katika bomu hilo lililolenga mapango na mahandaki ya chini kwa chini Mashariki mwa Afghanistan.

Kamanda wa kijeshi wa Marekani nchini Afghanistan, Jemedari John Nicholson, alisema kuwa Marekani iliamua kutumia bomu kubwa zaidi katika mashambulizi hayo kutokana na mbinu kambambe ya kijeshi.