Apple yapewa kibali cha magari ya kujiendesha

Kampuni ya Apple yapewa kibali cha magari ya kujiendesha

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kampuni ya Apple yapewa kibali cha magari ya kujiendesha

Kampuni ya Apple imepewa kibali cha kujaribu magari yake yanayojiendesha katika barabara za California.

Kumekuwa na habari kwamba kampuni hiyo imekuwa ikiandaa miradi ya gari la kujiendesha, ijapokuwa kampuni hiyo haijawahi kuthibtisha maelezo kama hayo.

Habari hizo zilitolewa hadharani na idara ya magari katika jimbo la California siku ya Ijumaa.

Idara hiyo imesema kuwa Apple imepewa idhini ya kujaribu magari matatu yaliotengezwa na Lexus.

Apple haijatoa tamko lolote isipokuwa kutaja kuhusu barua yake mwisho wa mwaka uliopita ikitaka kuanzisha teknolojia hiyo.

''Kampuni hiyo ilifurahia fursa ya mfumo wa magari katika maeneo mengi ikiwemo uchukuzi '',ilisema wakati huo.

Uvumi kuhusu hatua hiyo ya Apple kuhusu magari hayo ulianza kuhusu madai kwamba ilikuwa inatengeza gari lake hadi habari kwamba ilikuwa ikitaka kuangazia programu za magari.