Mtu mzee zaidi duniani afariki akiwa na umri wa miaka 117

Emma Morano amefariki akiwa umri wa miaka 117

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Emma Morano amefariki akiwa umri wa miaka 117

Mtu mzee zaidi duniani amefariki nchini Italia akiwa na umri wa miaka 117.

Emma Morano alizaliwa tarehe 29 mwezi Novemba mwaka 1899 eneo la Piedmont nchini Italia. Ndiye mtu wa misho aliyezaliwa miaka ya 1800 ambaye bado alikuwa hai.

Kuishi kwake miaka mingi kunatajwa kutokana na maumbile ya jeni na chakula chake ambacho ni mayai matatu kwa siku mawili yakiwa ni mabichi.

Bi Morano alikuwa kifungua mimba katika familia ya watoto wanane ambao wote washafariki.

Alifariki akiwa nyumbani kwake katika mji wa kaskazini wa Verbania.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Bi Morano akitazama picha yake akiwa mdogo

Alikiri kuwa kuishi kwake kulichangiwa na jeni kwa kuwa mama yake alifariki akiwa na umri wa miaka 91 na dada zeke nao waliishi miaka mingi.

Lakini pia alikuwa akila chakula kisicho cha kaiwada cha mayai matatu, mawili yakiwa mabichi kwa kipindi cha zaidi ya miaka 90.

Daktari wake wa miaka 27 Carlo Bava, aliambia AFP kuwa hakuwa akila mbona wala matunda

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Sherehe Bi Morano alipotimzia miaka 117 mwaka uliopita