Mlipuko wa bomu wawaua zaidi ya watu 100 Syria

Moshi uliotanda baada ya mlipuko Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Moshi uliotanda baada ya mlipuko

Gari lililokuwa limejaa mabomu likiendeshwa na mtu wa kujitolea mhanga limegongeshwa kwenye basi lililokuwa likiwahamisha raia wa Syria kutoka mji mmoja unaoshambuliwa.

Ripoti kutoka eneo hilo zinasema kuwa watu kadhaa waliokuwa kwenye basi hilo wamefariki hasa katika maeneo ya Aleppo na kwamba vipande vya miili yao vimeonekana kutapakaa kila mahali.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Waliojeruhiwa wakipelekwa hospitalini Alepo

Wachunguzi wa mambo yanayoendelea Syria wanasema kuwa zaidi ya watu 100 walifariki.

Msafara huo wa mabasi ulikuwa ukiwabeba wakaazi wa eneo hilo na wapiganaji wanaounga Serikali mkono kutoka vijiji viwili vya Washia chini ya mpango wa mapatano kati ya Serikali na waasi.

Image caption Syria

Wahamaji walichelewa kusafirisha kutokana na sintofahamu juu ya idadi ya waasi wanaopaswa kuruhusiwa kuondoka kutoka vijiji hivyo.

Licha ya mashambulizi hayo, ubadilishanaji wa raia na wapiganaji umerejelewa huku mabasi yakiingia katika maeneo yanayothibitiwa na Serikali na yale ya waasi.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Watu walikuwa wakisubiri kuabiri magari wakati mlipuko ulitokea