Bendeji za kutambua hali ya kidonda kufanyiwa majaribio

Bendeji za kutambua hali ya kidonda kufanyiwa majaribio
Maelezo ya picha,

Bendeji za kutambua hali ya kidonda kufanyiwa majaribio

Bendeji ambazo zinaweza kutambua jinsi kidondo kinapona na kutuma ujumbe kwa daktari itafanyiwa majaribio katika kipindi cha miezi 12 inayokuja.

Bandeji hizo zitatumia teknolojia ya 5G kufuatilia na kutambua ni matibabu ya aina gani yanahitajika kwa mgonjwa.

Majaribio hayo yanafanywa na taasisi ya Sayansi ya chuo cha Swansea.

Bendeji hii inatumia teknojia inayofahamika kama nano, kutambua hali ya kidonda cha mgonjwa wakati wote.

Kisha itainganisha kidonda na mfumo wa 5G kupitia kwa simu ya mkononi na kuonysha vitu kadha kuhusu mgonjwa, kama eneo alipo na hali yake.

Wakati taarifa hiyo yote inakuja pamoja , teknolojia hiyo kisha itatambua aina ya matibabu mgonjwa atahitaji.