Kiongozi wa kanisa katoliki Papa Francis aongoza maelfu kwa ibada St Peter's Square

Katika ibada ya kuamkia leo Papa Francis aliwahimiza waumini wasiwapuuze wahamiaji na maskini. Haki miliki ya picha AFP
Image caption Katika ibada ya kuamkia leo Papa Francis aliwahimiza waumini wasiwapuuze wahamiaji na maskini.

Maelfu ya mahujaji wamekusanyika Roma kushuhudia Papa Francis akiongoza ibada ya pasaka katika eneo la St Peter's Square.

Katika ibada ya kuamkia leo Papa Francis aliwahimiza waumini wasiwapuuze wahamiaji na maskini.

Ametoa ujumbe huu ukienda sambamba na shughuli wa kuwaoa zaidi ya watu 5,000 kutoka ngalawa mbovu zilizopatikana zikielea katika Ufuo wa Bahari ya Libya na Italia.

Papa Francis pia anatarajiwa kuzungumzia umuhimu wa mashauriano kati ya Madhehebu mbalimbali.

Matamshi hayo yanaonekana kulenga milipuko iliyotokea katika Kanisa la Coptic nchini Misri siku chache zilizopita.

Misa pia zilifanyika katika makanisa ya Coptic nchini Misri ambapo mashambulizi ya wiki iliyopita yalidaiwa kutekelezwa na Islamic State yaliwaua watu 45.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Maelfu ya wamehudhuria misa
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Papa Francis akiwa St Peter's Square
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ulinzi ulidumishwa
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Misa pia zilifanyika katika kanisa la Coptic nchini Misri