Uwanja wa ndege washambuliwa Mogadishu

Uwanja wa ndege washambuliwa Mogadishu

Chanzo cha picha, ABDULAZIZ BILLOW ALI

Maelezo ya picha,

Uwanja wa ndege washambuliwa Mogadishu

Taarifa kutoka Somalia zinaeleza kuwa mizinga kadha imerushwa dhidi ya uwanja wa ndege katika mji mkuu, Mogadishu.

Walioshuhudia tukio hilo, wanasema askari wa usalama wa Somalia, walipambana kwa risasi, na washambuliaji.

Inafikiriwa msha-mbu-liaji mmoja aliuwawa. Haijulikani nani alihusika na shambulio hilo.

Wakati huohuo, Shirika la Chakula Duniani, WFP, linasema kumetokea mlipuko mita mia moja kutoka msafara wake mjini Mogadishu.

WFP inachunguza kama mlipuko huo ulilengwa dhidi ya msafara wake.