Maelfu waokolewa Pwani ya Libya

Mtoto wa wiki mbili ni miongoni mwa walionusurika

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Mtoto wa wiki mbili ni miongoni mwa walionusurika

Maelfu ya wahamiaji wameokolewa baharini karibu na nchi ya Libya mwishoni mwa juma lililopita.

zaidi ya watu 2000 waliokolewa siku ya Ijumaa na 3000 siku ya jumamosi, ameeleza mwangalizi wa pwani ya Italia.

Lakini takriban watu saba wamezama baharini wakati ambapo waokoaji walipokuwa wakipambana kuwaokoa wahamiaji 1,500 katika Operesheni.

Mvulana mwenye umri wa miaka minane ni miongoni mwa waliopoteza maisha, waokoaji wameeleza.

Shirika la uokoaji Moas limesema limeokoa watu 453, lakini zaidi ya 1000 wako hatarini.

Shirika la madaktari wasio na mipaka, MSF limesema boti zake za uokoaji liliokoa takriban watu 1000 katika Operesheni siku ya Ijumaa.