Korea Kaskazini yaonywa na Marekani

Herbert Raymond McMaster aionya Korea Kaskazini
Maelezo ya picha,

Herbert Raymond McMaster aionya Korea Kaskazini

Mshauri wa Rais Donald Trump wa masuala ya usalama, Herbert Raymond McMaster amesema makubaliano yanayojitokeza dhidi ya tabia ya vitisho ya Korea Kaskazini kwa sasa yanaijumuisha China.

Katika mahojiano na shirika la habari la ABC General Mc Master amesema kuwa Marekani na China zinaelekea kupoteza uvumilivu na Korea Kaskazini

Amesisitiza kuwa majaribio ya makombora ya hivi karibuni,yanayonyesha tabia ya vitisho ya Korea Kaskazini,na nafikiri kuna makubaliano ya kimataifa sasa,ikiwemo China,kuhakikisha tabia hii haiendelei,na Rais Trump ameweka wazi kuwa Marekani na washirika wake hawatokubali kuona utawala wa vitisho dhidi ya silaha za nyuklia.

Makamu wa Rais wa Marekani Mike Pence,amefika Korea Kusini saa chache baada ya Korea Kaskazini kufanya jaribi lililokwama la uzinduzi wa makombora ya masafa ya mbali. Maafisa wa Marekano waliosafiri na kiongozi huyo wamesema kuwa walitarajia jaribio hilo lingekwama.

Akizungumza katika kambi ya jeshi Pence amesema uhuru utashinda.

'Fursa ya mimi kuwepo leo hapa kwa wakati kama huu,ni faida kubwa kwangu.Lakini ngoja niwahakikishie kuwa chini ya uongozi wa rais Trump,azimio letu chini ya watu wenye ujasiri wa Korea Kusini,haujawahi kuwa na nguvu,lakini kwa msaada wenu na Mungu uhuru utaendelea kuimarika katika rasi hii'.

Korea kaskazini imekuwa ikituhumiwa dhidi ya tishio la matumizi ya nyuklia.