Steve Stephens,muuaji anayesakwa Marekani

Steve Stephens muuaji anayesakwa Marekani
Maelezo ya picha,

Steve Stephens muuaji anayesakwa Marekani

Polisi katika jimbo la Ohio nchini Marekani wanamtafuta mtu anayedaiwa kufanya mauaji,huku akionyesha moja kwa moja mauaji hayo kupitia mtandao wa Facebook.

Maofisa katika mji wa Cleveland wamesema kuwa Steve Stephens anaonekana akionyesha moja kwa moja mauaji wakati akimpiga risasi mwanaume mmoja mtu mzima kupitia Facebook.

Mkuu wa Polisi mjini Cleveland Calvin Williams amemtaka Stephens ajisalimishe mwenyewe. Williams alisema kuwa mtu huyo ni hatari kuendelea kuwa mafichoni kwake.

Polisi wanasema hawajapata ushahidi madai ya Stephen kuwa amewauwa watu kumi na mmoja.