Recep Tayyip Erdogan apata ushindi mwembamba kura ya maoni

Recep Tayyip Erdogan apata ushindi mwembamba kura ya maoni
Image caption Recep Tayyip Erdogan apata ushindi mwembamba kura ya maoni

Mkuu wa bodi ya uchaguzi ya Uturuki ametangaza ushindi mwembamba wa Rais Recep Tayyip Erdogan anayetaraji kuwania muhula mwingine wa utawala. Kati ya Kura asilimia 99 zilizohesabiwa, Erdogan amepata kura za ndiyo asilimia 51.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Ankara mkuu wa Chama kikuu cha upinzani cha uturuki CHP Kemal Kilicdaroglu amehoji uhalali wa kura hiyo ya maoni .

"Tumefanya kura ya maoni katika mazingira yasiyo na usawa. Kila mtu anafahamu kuhusu hilo"

Kilicdaroglu amependekeza kuwepo masuala ya kisheria katika matokeo ya kura hiyo ya maoni kwa kusema kuwa wanaheshimu maamuzi ya watu, lakini yamegubikwa na bodi ya juu ya uchaguzi. Kura hii ya maoni imezua mjadala wa wazi kwa misingi ya kisheria na kwa nisingi ya maadili ya watu.

Wanasiasa wanahoji kura ya maoni na taratibu zake.

Huu ni ushindi mwembamba, kinyume na matarajio aliyokuwa nayo bwana Rais Recep Tayyip Erdogan katika kura hii ya maoni.