Gwaride la kusisimua lafanyika Korea Kaskazini

'Siku ya jua' mjini Pyongyang iliadhimishwa kwa maonyesho ya makombora, mwendo bila kukunja magoti na mapambo ya nguo (pom-poms)

Wanajeshi wa Korea Kaskazini katika maadhimisho ya 105 ya kuzaliwa kwa rais mwanzilishi wa taifa hilo.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Korea Kaskazini imeandaa gwaride kubwa na la kusisimua katika mji mkuu Pyongyang kuadhimisha miaka 105 tangu kuzaliwa kwa kiongozi mwanzilishi wa taifa hilo, Kim Il-sung.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Maadhimisho hayo yanajulikana kama 'Day of the Sun' ama siku ya jua, kwani Kim Il-sung mara nyingi huwa anatambulishwa kwa ishara jua.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Maadhimisho hayo yalionekana kama maonyesho ya nguvu za kijeshi wakati kumekuwa na uhusiano baridi baina ya Marekani na Korea Kaskazini.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Mwandishi wa BBC aliyehudhuria maadhimisho hayo anasema kwamba alihisi ardhi ikitetemeka wakati wanajeshi walipokuwa wakipita pamoja na makombora.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Wanajeshi wanawake wakitembea bila kukunja magoti katika onyesho la kusisimua.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Bendera ya Korea Kaskazini ilipeperushwa kwa nguvu.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Kundi la wanaume wakiwa wamebeba mapambo yanayowekwa kwenye nguo ama kofia (pom-poms)

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Ndege angani zimeunda umbo la takwimu 105.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Kiongozi wa Korea Kusini Kim Jong-un, mjukuu wa rais mwanzilishi wa taifa hilo, awapungia mkono watu waliohudhuria maadhimisho hayo.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Mwanajeshi apiga picha za maadhimisho hayo.