John Terry kuondoka Chelsea mwisho wa msimu

Nahodha wa klabu ya Chelsea John Terry akiwa na mpenziwe
Maelezo ya picha,

Nahodha wa klabu ya Chelsea John Terry akiwa na mpenziwe

Nahodha John Terry pamoja na klabu ya Chelsea kwa pamoja wametangaza kuwa mchezaji huyo ataondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu.

Kila mtu katika uwanja wa Stamford Bridge angetaka kuonyesha shukran kwa John na kumuombea heri katika siku za usoni.

''John ametufanyia kazi kubwa na ya kujitolea ''.

Katika muda wote ameonyesha uzalendo wake akivalia jezi ya Chelsea kitu ambacho amekifanya mara 713 tangu aingie Chelsea 1998, akifunga magoli 66.

Ni mchezaji wa tatu kwa kushiriki mechi nyingi za klabu hiyo na amekuwa nahodha wa klabu hiyo kwa rekodi ya mara 578.

Msimu huu hajashirikishwa sana licha ya kuwa na ushawishi mkubwa miongoni mwa wachezaji wengi wa klabu hiyo ambayo chini ya uongozi wa Antonio Conte bado inaongoza jedwali la ligi.