Muda wa tangazo la hali ya hatari waongezwa Uturuki

Rais Recep Tayyip Erdogan atangaza muda zaidi wa hali ya hatari
Maelezo ya picha,

Rais Recep Tayyip Erdogan atangaza muda zaidi wa hali ya hatari

Serikali ya Uturuki imesema kuwa imeongeza ukomo wa ongeza tangazo la hali ya hatari nchini humo kwa miezi mingine mitatu.Hali ya hatari nchini humo awali ilitangazwa kutokana na jaribio la mapinduzi mwezi July,ambapo tangazo hili la sasa limekuja siku moja tu baada ya rais wa taifa hilo Recep Tayyip Erdogan kupata ushindi mwembamba katika hatua yake ya kutaka kuongeza muda wake madarakani.

Mapema Erdogan alisema kuwa atapuuza ukosoaji wa kimataifa katika kura ya maoni iliyofanyika siku ya jumapili,akizungumza na waangaliazi wa kimtaifa alisema kuwa wanapaswa kufahamu nafasi yake.Amesisitiza kuwa angelishikilia kura ya maoni kwa zaidi ya muongo mmoja wa mazungumzo kuhusiana na kujiunga na jumuiya ya Ulaya.

Hata hivyo maandamano yalianza mara tu baada ya upigaji kura huo.Murat Kazanci ni muandamanaji kutoka mjini Istanbul anasema matokeo ni ya uongo

"Na amini kulikuwa na mchezo mchafu na matukio mengi ya ukiukaji wa sheria.Tulisikia habari nyingi.Tulisimama kidete kwaajili ya kura yetu siku ile,hatukubaliani na kura ya ndiyo kwa sababu matokeo ilikuwa ni kura ya hapana.

Haya ndiyo matokeo ya maandamano haya,anasema Bi. Yasar Bodur na kusisitiza kwamba kwanini anaandamana

Hapo jana rais wa sasa wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ametangazwa kuwa mshindi kwa asilimia 51 katika kura ya maoni iliyopigwa nchini humo,ushindi unaotajwa kuwa ni mdogo baada ya kupata kiwango kidogo na kwamba Erdogan mwenyewe hakutegemea matokeo hayo.