Raia wa Cameroon Vera Songwe apewa wadhifa UN

Vera Songwe ndiye mwanamke wa kwanza kuteuliwa kama Katibu Mkuu wa Tume ya Uchumi barani Afrika (ECA)

Chanzo cha picha, UNIDO

Maelezo ya picha,

Vera Songwe ndiye mwanamke wa kwanza kuteuliwa kama Katibu Mkuu wa Tume ya Uchumi barani Afrika (ECA)

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres alimteua Vera Songwe ambaye ni mwanauchumi kutoka Cameroon kuwa katibu mkuu wa Tume ya Uchumi barani Afrika (ECA) na atakuwa mwanamke wa kwanza kuwahi shikilia nafasi hii.

Bi Songwe anachukua usukani kutoka Carlos Lopes mkaazi wa Guinean-Bissau ambaye alijiuzulu.

Guterres alimteua Bi Songwe ambaye ana umri wa miaka 42 kutoka Benki ya Dunia ambako alikuwa akifanya kazi tangu 1998.

Bi Songwe amekuwa akifanya kazi kama mwakilishi mkazi katika Shirika la fedha la Kimataifa (IFC) akishughulikia masuala ya uwekezaji fedha za kibinafsi tangu 2015.

Kati ya miaka 2011 na 2015, Vera Songwe alihudumu kama Mkurugenzi wa uendeshaji katika benki ya Dunia nchini Senegal, Cape Verde, The Gambia, Guinea Bissau na Mauritania.