Mwanamke ambaye simu yake ilimpatia matokeo ya makosa ya HIV

Simu aina ya smartphone ilitengezwa ili kumwezesha mtumiaji wake.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Simu aina ya smartphone ilitengezwa ili kumwezesha mtumiaji wake.

Esther huuza maji kandakando ya barabara nchini Kenya kwa dola chache kwa siku.

Pia anamiliki simu aina ya smartphone na kumiliki kifaa hicho kulingana na washauri wengi ni kumwezesha mmiliki wake.

Lakini badala yake simu hiyo haikumsaidia alipopata programu.

Ilidai kutoa matokeo yake ya HIV kwa kuchanganua alama zake za vidole katika skrini yake.

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha,

Wanawake na wasichana nchini Kenya wana bahati kubwa ya kupata simu ikilinganishwa na wanaume lakini hatua hiyo huja na gharama

Wakati watafiti walipokutana naye katika kibanda chake cha kazi alikuwa na wasiwasi.

Hakujua iwapo ilikuwa ukweli na alikuwa na wasiwasi mwingi, alisema mtafiti Laura de Reynal, ambaye alifanya kazi kama mtafiti wa uzoefu wa mtu anayetumia simu za smartphone kwa mara ya kwanza.

''Na hakuwa yeye pekee, kulikuwa na wengine ambao walikuja kwetu wakiwa na wasiwasi na ni hao pekee walikuwa wakiweza kuzungumza nasi''.

Programu hiyo hatahivyo ilidaiwa kuwa mzaha na mtu yeyote aliyesoma maoni katika google wanaona hilo.

Hatahivyo wanaomiliki simu hiyo kwa mara ya kwanza nchini Kenya walipata programu hizo kutoka kwa simu za rafiki zao kupitia programu ya Blue Tooth badala ya kuzipakuwa kutoa mtandao ili kuhifadhi data.

Chanzo cha picha, Mozila

Maelezo ya picha,

Kujifunza mbinu ya kukamiliana na uhalifu wa mtandaoni

Hatahivyo mzaha huo haungedhihirika kupitia kusambazwa kwake katika bluetooth.

Ukizinduliwa na Morzila, chini ya mfumo wa Firefox, utafiti huo ulilenga kubaini ni nini haswa kinawazuia watu wanaoishi katika mataifa yanayaoendelea kuchukua fursa inayotolewa na mtandao.

Utafiti huo ulibaini kwamba wanaume hudhibiti viwango vya mtandao unaotumiwa na wanawake.

Pia umedai kwamba kutumiaa mtandao bila ya mafunzo pia huchangia mambo mabaya katika mtandao kama vile uchezaji wa kamare.

Swala hilo la Esther limewafanya watafiti kuzungumza na Google kuweka onyo katika programu hizo ili kuweza kukabiliana na vikwazo vya lugha.

Mtandao huo umeandikwa Kiingereza huku watumiaji wapya nchini Kenya wakizungumza kiswahili na sheng -lugha iliochanganyika na kiswahili pamoja na Kiingereza.

"Vifaa hivyo hutengezwa katika eneo la Sicon Valley ambapo utumizi wake hufanyika'', alisema Bi de Reynal.

''Wanaweza kuwa na vipengee vinavyobadili yaliomo kwa lugha ya kinyumbani, kwa mfano'',alisema.

Samantha Burton aliyesisimamia mradi huo alikubali.

Chanzo cha picha, Mozilla

Maelezo ya picha,

Simu aina ya smartphone

''Kuweka smartphone katika mikono ya mtu hakumaanishi kumuwezesha moja kwa moja , watumiaji wapya hutakikana kutumia vifaa vipya'', alisema.

Jibu la wazi ni kuwaelimisha kuhusu mfumo wa dijitali ili kujibu maswali kuhusu utumiaji wa data, kuweka neno la siri mbali na kubaini habari bandia na uhalifu mwengine wa mtandaoni.

Lakini watu ambao wako tayari kufanya lolote ili kupata dola moja kuna uwezekano mkubwa huenda wasipate muda wa kuwa na mikutano kama hiyo.

''Sababu kuu ya watu kumiliki simu ya smartphone ni mawasiliano, kutumia facebook ama hata whatsApp-kwa hivyo hatua ya kuwataka watu kuzungumza haikuwa na umaarufu wowote'' alisema Bi Burton.

Faith ambaye ni mfanyibiashara mjini Nairobi hutumia simu yake ya rununu kununua na kuuza bidhaa katika mtandao na kutafuta programu za kuwatumbuiza watoto wa shule za kanisani siku ya Jumapili.

Lakini kama wanawake wengine hakuweza kuimiliki simu hiyo.

Baada ya kukosana na mpenziwe alipokonywa simu na kulazimika kununua yake.

Simu hiyo ilionunuliwa kutoka kwa binamu yake nchini Rwanda, haikufanya kazi na Faith hakujua kuitengeza.

Wanawake nchini Kenya wana uwezo mara tatu kupewa simu ya smartphone kama zawadi kutoka kwa wanaume katika maisha yao ,ambao pia huangalia huduma zao za whatsApp.

Simu ya rununu ni kitu kikubwa miongoni mwa Wakenya masikini.