Harry Redknapp ndiye kocha mpya wa Birmingham City

Kocha mpya wa Birmingham Harry Rednapp Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kocha mpya wa Birmingham Harry Rednapp

Klabu ya Birmingham City imemuajiri Harry Reknapp kuwa meneja wake mpya.

Kocha huyo wa zamani wa West Ham, Tottenham na QPR anachukua mahali pake Gianfranco Zola aliyejiuzulu siku ya Jumatatu baada ya kushindwa 2-0 na timu ya daraja la kwanza nchini Uingereza Burton Albion.

Blues wako katika nafasi ya 20 katika jedwali , pointi tatu juu ya eneo la kushushwa daraja ikiwa imesalia mechi tatu na watacheza dhidi ya Aston Villa siku ya Jumapili.

''Birmingham ni klabu nzuri lakini iko katika nafasi mbaya'' ,alisema Rednapp mwenye umri wa miaka 70.

Alichukua ukufunzi wa taifa la Jordan katika mechi mbili za kufuzu kwa kombe la dunia mwaka uliopita, ambapo alifanya kazi kama mshauri wa Derby County msimu uliopita, lakini hajaifunza Uingereza tangu aondoke QPR mnamo mwezi Februari 2015.

Akiwa mshindi wa kombe la FA na klabu ya Portsmouth 2008, aliiongoza Tottenham kufika robo fainali ya mashindano ya vilabu bingwa Ulaya akiwa mkufunzi wa klabu hiyo kwa takriban miaka minne.

Mwaka 2016, alifanywa kuwa mkurugenzi katika klabu ya Wimbornena na baadaye mshauri wa soka wa timu ya Central Coast mariners nchini Australia.