Korea Kaskazini inaaminika kumiliki zaidi ya silaha 1000 zenye uwezo tofauti

Uwezo wa Makombora ya Korea Kaskazini
Maelezo ya picha,

Uwezo wa Makombora ya Korea Kaskazini

Korea kaskazini inaaminika kumiliki zaidi ya silaha 1000 zenye uwezo tofauti ikiwemo kombora la maasafa marefu ambalo linaweza kuishambulia Marekani.

Mpango wa Pyongyang umeendelea katika miongo kadhaa ya hivi karibuni kutoka mizinga mikubwa katika miaka ya tisini na sabini hadi makombora ya masafa mafupi mbali na yale ya masafa marefu katika miaka 80 na 90.

Mifumo ilio na uwezo mkubwa inadaiwa kufanyiwa utafiti.

Hivi karibuni, Korea Kaskazini ilitangaza kwamba inaunda makombora ya masafa marefu yanayoweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine ambayo yanaweza kushambulia mataifa ya magharibi.

Taifa la Korea Kaskazini linaaminika kutengeza kombora la masafa marefu zaidi ambalo wachunguzi wamelitaja kuwa KN-08 ama Hwasong-13.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Makombora ya Hwasong yakiwa katika maonyesho

Ishara za kwanza kuhusu utengenezaji huo ulifanyika Septemba 2016 ambapo taifa hilo lilifanyia majaribio mashine mpya ya roketi ambayo baadhi ya watu wanasema inaweza kurusha kombora kutoka bara moja hadi jingine.

Idara ya ulinzi nchini Marekani Pentagon inaamini kwamba Korea Kaskazini inamiliki makombora 6 aina ya KN-08, ambalo lina uwezo wa kufika hadi Marekani.

Korea kaskazini inaaminika kutengeza toleo jipya la kombora hilo linalojulikana kama KN-14.

Haahivyo makombora hayo hayajafanyiwa majaribio.

Lakini mnamo mwezi Januari 2017, kulikuwa na ishara ya jaribio, muda mfupi baada ya kiongozi Kim Jong un kudai kwamba taifa hilo lilikuwa katika awamu ya mwisho ya kutengeza kombora la masafa marefu linaloweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine.

Mpango wa kisasa wa kutengeza makombora yaa Korea Kasakzini ulianza kwa kutengeza makombora ya scud ambapo yalipitia Misri mwaka 1976.

Kufikia 1984, taifa hilo lilikuwa likitengeza makombora yake kwa jina Hwasong.

Inaaminika kuwa na makombora tofauti tofauti ya masafa mafupi ambayo yanaweza kulenga taifa jirani la Korea Kusini.

Uhusiano kati ya mataifa hayo mawili ya Korea umeharibika na yamekuwa yakijiandaa kukabiliana kivita.

Kombora la Hwasong 5 na Hwasong 6 ambayo pia hujulikana kama Scud B na Scud C yana uwezo wa kwenda kilomita 300 na 500 mtawalia kulingana na kituo cha Marekani kinachofanya utafiti wa kuzuia kuenea kwa nuklia.

Makombora hayo yanaweza kubeba makombora ya kemikali na nyuklia.

Silaha hizo zimejaribiwa na kupelekwa katika maeneo yanayohitajika na kombora la Hwasong-6 limeuzwa nchini Iran.

Maelezo ya picha,

Ramani ya Korea Kaskazini na majirani zake wa Korea Kusini

Korea Kaskazini ilianza mpango huo mapema miaka ya 80 kutengeza kombora la masafa ya kadri kwa jina Nodong likiwa na uwezo wa kusafiri urefu wa kilomita 1000.

Kombora hilo limetengezwa kwa muundo wa Scud ,lakini ni asilimia 50 kwa ukubwa na lina mashine yenye uwezo mkubwa.

Uchanganuzi wa mwezi Aprili 2016 wa taassii ya kimataifa kuhusu utafiti wa mikakati ,unasema kuwa makombora hayo yalithibtishwa yanaweza kupiga maeneo yote ya Korea Kusini na Japan.

Imeongezea kuwa maonyesho ya Oktoba 2010 yalithibitisha kuwa kombora hilo linaweza kufika urefu wa kilomita 1,600 ikimaanisha kwamba linaweza kupiga kambi kadhaa za Marekani zilizopo katika eneo la Okinawa.

Makombora hayo ya Nodong yanadaiwa kujaribiwa 2006, 2009, 2014 na 2016.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Kombora la Musudan

Korea Kaskazni imekuwa ikitengeza makombora ya Musudan kwa miaka kadhaa, na hivi karibuni ilifanya majaribio 2016.

Makadirio yanatofautiana kuhusu viwango vyake, huku ujasusi wa Israel ukitaja uwezo wake kuwa kilomita 2,500 nacho kitengo cha ulinzi wa makombora nchini Marekani kikikadiria kuwa na uwezo wa kufika kilomita 3,200.

Duru nyengine zinasema kuwa kombora hilo lina uwezo wa kwenda kilomita 4,000.

Kombora la masafa mafupi la Musudan ambalo pia linajulikana kama Nodong B ama Taepodong-x linaweza kulishambulia taifa lote la Korea Kusini na Japan.

Kombora hilo linaweza kushambulia kambi za kijeshi za Marekani katika eneo la Guam.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Kombora la masafa marefu la Taepodong linaloweza kurushwa kutoka bara moja hadi jingine

Korea Kaskazini inasema kuwa imefanyia majaribio kombora la masafa ya kadri, kwa jina Pukguksong, mnamo mwezi Agosti 2016 likirushwa kutoka kwa manuwari.

Kombora la pili lilirushwa kutoka ardhini mnamo mwezi Februari 2017.

Pyongyang ilisema kuwa ilitumia mafuta ,na kufanya kuwa rahisi kuliwasilisha na kurusha.

Hatahivyo maelezo kuhusu uwezo wake hayajulikani.