Bi.May ataka utulivu wa kisiasa Uingereza

Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May
Maelezo ya picha,

Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May

Waziri mkuu wa Uingereza, Theresa May anasema tangazo lake la uchaguzi wa mapema ni njia pekee ya kuhakikisha utulivu wakati nchi inazungumzia kujiondoa kutoka umoja wa ulaya.

Bi May anaenda katika Bunge kuwaomba wabunge waunge mkono uamuzi wa kwenda kwenye uchaguzi mwezi Juni miaka mitatu mapema kabla ya ratiba ya awali.

Anategemea kupata uungwaji mkono anaoutaka. Kura za maoni zinawaweka konsevativu pointi ishirini mbele ya wapinzani wakuu Labour Party. Kiongozi wa Labour, Jeremy Corbyn alisema alikuwa akiangalia mbele kuelekea kampeni.