UN yathibitisha makaburi ya pamoja DRC

Nchi hiyo imekumbwa na eneo la mashariki, na hivi karibuni eneo la Kasai magharibi mwa nchi Haki miliki ya picha AFP
Image caption Mwanajeshi katika Jmauhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Makaburi ya pamoja 17 yamepatikana katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na idadi hiyo sasa imefika 40. Hii ni kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa .

Makaburi haya yamepatikana katika eneo la Kasai ambapo kumekua na makabiliano kati ya wapiganaji wa kundi la Kamuina Nsapu na majeshi ya serikali ya Congo.

Waasi hao walianza kupambana na jeshi la serikali baada ya kiongozi wao kuuawa.

Image caption Ramani ya DRC

Pande zote mbili zimelaumiwa kwa kukiuka haki za kibinadamu.

Wachunguzi wa Umoja wa Mataifa wamesema takriban watu 74 wakiwemo watoto 30 waliuwawa katika vita hivyo mwisho wa mwezi uliopita.

Afisa Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya haki za binadamu Ra'ad Al Hussein ametaka mamlaka katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuchunguza visa vya ukiukaji wa haki za binadamu akisema pande hasimu zimehusika na ukatili wa kibinadamu katika eneo la Kasai.

Mada zinazohusiana