Buhari amfuta kazi mkuu wa ujasusi

Dola milioni 43 (£33m) pesa taslimu ilipatikana katika nyumba iliyo eneo la matajiri wiki iliyopita. Haki miliki ya picha EFCC
Image caption Dola milioni 43 (£33m) pesa taslimu ilipatikana katika nyumba iliyo eneo la matajiri wiki iliyopita.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amemuachisha kazi kwa muda mkuu Shirika la Ujasusi, Ayo Oke, na kuamuru uchunguzi ufanywe baada ya dola milioni 43 (£33m) pesa taslimu kupatikana katika makaazi yake mjini Lagos.

Pesa hizo ambazo zilipatikana na Shirika la kupambana na ufisadi kufuatia kidokezo kutoka umma.

Bwana Buhari ameamuru wachunguzi kubaini vipi NIA ilipokea fedha hizo na kudhibitisha iwapo walivunja sheria.

Taarifa kutoka kwa Rais imesema kamati inayoongozwa na Naibu Rais itafanya uchunguzi na kupeana ripoti yao kwake katika siku 14 zijazo.

Mada zinazohusiana