Maelfu waandamana Venezuela dhidi ya serikali

Upinzani unataka kufanyike uchaguzi wa Urais Haki miliki ya picha EPA
Image caption Waandamanaji Venezuela

Maelfu ya raia wa Venezuela wameandamana katika mji mkuu wa Caracas na katika miji mingine zaidi ya 20. Waandamanaji wanataka kufanyike uchaguzi wa Urais na kuachiliwa huru kwa wanasiasa wa upinzani.

Wafuasi wa Rais Nicolas Maduro pia wamekua wakiandamana katika mji mkuu wa Caracas, kama ishara ya kumuunga mkono kiongozi huyo.

Licha ya kuwa na utajiri mkubwa wa mafuta, Venezuela imeendelea kukumbwa na mfumuko mkubwa wa bei, visa vingi vya uhalifu na uhaba wa bidhaa muhimu.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wafuasi wa serikali wakiandamana Venezuela

Upinzani umelaumu serikali yenye kufuata mfumo wa ujamaa kwa matatizo ya sasa ya kiuchumi.

Msukosuko wa sasa wa kisiasa ulichochewa na hatua ya Mahakama ya Juu kutwaa mamlaka ya bunge ambalo linathibitiwa na upinzani.

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Mwandamanaji Venezuela

Hata hivyo Mahakama ya Juu ilibatilisha uwamuzi wake baada ya kuzuka maandamano.

Kwa sasa Venezuela inashuhudia maandamano makubwa zaidi kuwahi kutokea kwa miaka mitatu

Mada zinazohusiana