Upinzani Venezuela kuandamana tena

kumekua na mapambano kati ya waandamanaji na Vikosi vya kuzuia ghasia Haki miliki ya picha Reuters
Image caption kumekua na mapambano kati ya waandamanaji na Vikosi vya kuzuia ghasia

Ghasia na kufyatua risasi kulijitokeza baada ya mamia ya raia wa Venezuela walipoandamana mitaani wengine wakimuunga mkono rais Nicolas Maduro na wengine wakiipinga serikali.

Polisi wa kuzuia ghasia walitumia gesi ya kutoa machozi na risasi za mpira kuwatawanya wapinzani mjini Caracas, ambapo kijana mmoja alipigwa risasi na kupoteza maisha.

Katika Mji wa magharibi mwa nchi hyo San Cristobal, mwanamke mmoja aliuawa mara baada ya maandamano kugeuka vurugu.

Upinzani unataka uchaguzi mpya wa urais kutokana na kudorora kwa uchumi nchini humo.

Rais Maduro ameulaumu upinzani kwa kusababisha vurugu.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Rex Tillerson amesema rais Maduro anakiuka Katiba ya Venezuela

Wapinzani wa rais wa Venezuela, Nicolas Maduro wameitisha maandamano mapya siku ya Alhamisi, siku moja baada ya kutokea ghasia.

Kiongozi mkuu wa upinzani Henrique Capriles amezungumza na waandishi wa habari kuwa siku ya leo watakutana raia wote wa Venezuela wakiwa na lengo la kushinikiza rais Maduro kuondoka madarakani.