Juventus yaiondoa Barcelona robo fainali

Baadhi ya wachezaji wa Barcelona wakiwa katika mshangao wa matokeo
Image caption Baadhi ya wachezaji wa Barcelona wakiwa katika mshangao wa matokeo

Juventus ambao mara ya mwisho walishinda Champions League mwaka 1996 wame watupa Barcelona nje ya Champions League. Barcelona wameshindwa kuushangaza tena ulimwengu wa soka kama walivyofanya katika hatua ya 16 bora pale walipoipiga Paris St-Germain bao 6-1 ingawa PSG ilikuwa na bao nne kibindoni.

Sasa Juventus wanaungana na Real Madrid, Atletico Madrid na Monaco katika droo itakayotangazwa kesho.

Monaco nayo imeingia hatua ya nusu fainali kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2004 baada ya jana kuwabamiza Borussia Dortmund bao tatu kwa moja.