Francois Hollande kuitisha baraza la Usalama

Rais wa Ufaransa Francois Hollande amesema wako katika hali ya tahadhari Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais wa Ufaransa Francois Hollande amesema wako katika hali ya tahadhari

Rais wa Ufaransa Francois Hollande ameahidi kuitisha mkutano wa baraza lake la masuala ya usalama, Ijumaa asubuhi.

Ametoa salamu za rambirambi kwa Familia za waathirika wa mashambulizi na kuahidi ushirikiano na kuwahakikishia huduma za usalama.

Kutokana na tukio hilo wagombea urais 11 wameonyesha kuguswa na tukio hilo huku wagombea wawili Marine le Pen na Francois Filon wakiahirisha kampeni zao hii leo.