Diamond Platinumz azindua manukato Tanzania

Manukato hayo yamepewa jina Chibu Perfume Haki miliki ya picha Diamond Platinumz / Instagram
Image caption Manukato hayo yamepewa jina Chibu Perfume

Mwanamuziki mashuhuri nchini Tanzania Diamond Platinumz amepiga hatua nyingine baada ya kujitosa katika biashara ya uuzaji wa manukato.

Manukato ya mwanamuziki huyo yamepewa jina Chibu Perfume, kwa kufuata jina lake ya utani la Chibu Dangote.

Chupa ya manukato hayo inauzwa takriban Sh105,000 za Tanzania.

Diamond anaonekana kuwafuata wasanii wengine mashuhuri duniani ambao wamejiingiza katika biashara ya manukato na hutumia umaarufu wa nembo zao kujipatia mapato zaidi.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii