Marekani kuchukua wakimbizi 1200 kutoka Australia

Donald Trump na waziri mkuu wa Australia Turnbull
Image caption Donald Trump na waziri mkuu wa Australia Turnbull

Makamo wa rais wa Marekani, Mike Pence, amethibitisha kuwa Marekani itatimiza ahadi iliyotolewa na rais msataafu, Rais Obama, kwamba Marekani itapokea wakimbizi 1200 kutoka kambi za wakimbizi nchini Australia.

Akizungumza baada ya mazungumzo na waziri mkuu wa Australia, Malcolm Turnbull, mjini Sydney, Bwana Pence alisema, wale wanaotaka hifadhi Marekani, watakabiliwa sheria kali za ukaguzi.

Makubaliano hayo kuhusu wakimbizi, yalisababisha mzozo kwenye simu baina ya Bwana Turnbull na Rais Trump mwezi wa Februari, ambapo Rais Trump alielezea makubaliano hayo kuwa ya kijinga.

Bwana Pence alisema Marekani itachunguza makubaliano hayo, lakini itayatekeleza, kwa sababu ya kuheshimu umuhimu wa urafiki kati ya nchi mbili hizo.