Maandamano ya kuunga mkono sayansi yafanyika duniani

Waandamanji wakiunga mkono sayansi
Image caption Waandamanji wakiunga mkono sayansi

Mihadhara ya kuunga mkono sayansi inafanywa katika miji zaidi ya 500 sehemu mbalimbali za dunia.

Hiyo ndiyo mihadhara ya mwanzo kutetea sayansi, iliyoanza New Zealand na Australia, ambako maelfu walishiriki kupinga kile wanachoona kuwa mashambulio yanayozidi ya wanasiasa, kupinga ukweli na ushahidi.

Baadhi yao walivaa makoti meupe ya maabara, na kubeba mabiramu kusema, "tunataka watu wanaotafakari siyo wanaokanusha' .

Waliopanga shughuli hiyo kimataifa, wanasema kilichowachochea kuchukua hatua, ni mipango ya Rais Trump kupunguza sana bajeti za idara za sayansi za Marekani.

Wanasema sayansi ni msingi wa maisha ya kawaida, haifai kuidhoofisha.