Wake wa polisi waandamana mjini Paris

Wake wa maafisa wa polisi waandamana Paris Ufaransa Haki miliki ya picha AFP/Getty
Image caption Wake wa maafisa wa polisi waandamana Paris Ufaransa

Zaidi ya wake 100 na washirika wao wamefanya maandaamno wakipinga mashambulio dhidi ya maafisa wa polisi kufuatia kuuawa kwa afisa mmoja huko Elysee.

Wake hao waliokuwa na ghadhabu waliandaman katikati ya mji siku mbili baada ya xavier Jugele alipigwa risasi mara mbili katika kichwa na muhalifu karim Cehurfi.

Wakati huohuo vyombo vya habari nchini Ufaransa vinasema kuwa mtu alikuwa akijihami na kisu amekamatwa katika eneo la gare du Nord.

Polisi hawajasema iwapo kisa hicho ni cha kigaidi.

Ufaransa inashiriki katika uchaguzi mkuu siku ya Jumapili.

Kwengineko maafisa wa polisi walikabiliana na waandamanaji baada ya maandamano ya muungona wa wafanyikazi mashariki mwa Paris, mabo walitaka kura ya awamu ya kwanza.

Maafisa wa polisi walirushiwa vitu nao wakalipza kuptia gesi za kutoa machozi.