Ufaransa yamchagua rais mpya

Police officers patrol in Paris Haki miliki ya picha AFP / Getty Images
Image caption Karibu polisi 50,000 na wanajeshi 7,000 wametumwa kote nchini

Raia wa Ufaransa wanapiga kura ya urais hivi leo.

Kwa mara ya kwanza baada ya miongo kadhaa , huu umekuwa uchaguzi usiotabirika.

Takriban asilimia 30 ya wapiga kura wanaaminika kwamba hawajatangaza msimamo wao.

Wawaniaji watatu wakuu hawana historia yoyote ya kisiasa akiwemo Emmanuel Macron, Marine le Pen na Jean-Luc Melenchon

Mpinzani wao mhafidhina Francois Fillon, amehudumia serikali katika nyadhfa kadhaa za uwaziri katika kipindi cha miongo miwili.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wagombea maarufu (Kushoto kuenda kulia): François Fillon, Benoît Hamon, Marine Le Pen, Emmanuel Macron na Jean-Luc Mélenchon

Hakuna yeyote anayetarajiwa kuibuka na ushindi katika duru ya kwanza, na wawili watakaoongoza uchaguzi huo watamenyana na katika duru ya pili mwezi ujao.

Usalama umeimarishwa kufuatia shambulizi la kigaidi lililotokea katikati mwa mji mkuu Paris alhamis, ambapo afisa mmoja wa polisi aliuwawa.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Baadhi ya wapiga kura walio nchi za nje tayari wamepiga kura zao